Zaburi 71:19-24 NEN

Zaburi 71:19-24

71:19 Lk 1:49; Za 36:5; 35:10; 77:13; 89:8; 126:2Ee Mungu, haki yako imefika juu katika mbingu,

wewe ambaye umefanya mambo makuu.

Ee Mungu, ni nani aliye kama wewe?

71:20 Za 80:3, 19; 25:17; 85:4; 63:9; Hos 6:2Ingawa umenifanya nipate taabu, nyingi na chungu,

utanihuisha tena,

kutoka vilindi vya dunia

utaniinua tena.

71:21 Za 18:35; 86:17; Isa 12:1; 40:1, 2; 49:13; 54:10Utaongeza heshima yangu

na kunifariji tena.

71:22 Za 33:2; 92:3; 144:9; Ay 21:12; 2Fal 19:22Ee Mungu wangu, nitakusifu kwa kinubi

kwa ajili ya uaminifu wako;

Ee Uliye Mtakatifu wa Israeli,

nitakuimbia sifa kwa zeze.

71:23 Za 20:5; Kut 15:13Midomo yangu itapaza sauti kwa furaha

ninapokuimbia sifa,

mimi, ambaye umenikomboa.

71:24 Za 35:28; Es 9:2Ulimi wangu utasimulia matendo yako ya haki

mchana kutwa,

kwa maana wale waliotaka kunidhuru,

wameaibishwa na kufadhaishwa.

Read More of Zaburi 71