Zaburi 71:1-8 NEN

Zaburi 71:1-8

Zaburi 71

Kuomba Ulinzi Na Msaada Siku Zote Za Maisha

71:1 Kum 23:15; Rut 2:12; Za 22:5Ee Bwana, nimekukimbilia wewe,

usiache nikaaibika kamwe.

71:2 2Fal 19:1671:2 Kut 34:6Kwa haki yako uniponye na kuniokoa,

unitegee sikio lako uniokoe.

71:3 Za 18:2Uwe kwangu mwamba wa kimbilio,

mahali nitakapokimbilia kila wakati;

toa amri ya kuniokoa, kwa kuwa wewe

ni mwamba wangu na ngome yangu.

71:4 2Fal 19:19; Za 140:4; Mwa 48:16Ee Mungu wangu uniokoe kutoka kwenye mkono wa mwovu,

kutoka kwenye makucha ya watu wabaya na wakatili.

71:5 Za 9:18; 25:5; Ay 4:6; Yer 17:7Kwa kuwa umekuwa tumaini langu, Ee Bwana Mwenyezi,

tegemeo langu tangu ujana wangu.

71:6 Ay 3:16; Za 9:1; 22:9; 34:1; 52:9; 119:164; 145:2Tangu kuzaliwa nimekutegemea wewe,

ulinitoa tumboni mwa mama yangu.

Nitakusifu wewe daima.

71:7 Kum 28:46; 1Kor 4:9; Za 61:3; 2Sam 22:3Nimekuwa kama kioja kwa wengi,

lakini wewe ni kimbilio langu imara.

71:8 Za 71:15; 51:15; 63:5; 96:6; 104:1Kinywa changu kimejazwa sifa zako,

nikitangaza utukufu wako mchana kutwa.

Read More of Zaburi 71