Zaburi 7:10-17 NEN

Zaburi 7:10-17

7:10 Za 3:3; Ay 33:3Ngao langu ni Mungu Aliye Juu Sana,

awaokoaye wanyofu wa moyo.

7:11 Mwa 18:25; Za 9:8; 67:4; 75:2; 96:13; 98:9; Isa 11:4; Yer 11:20Mungu ni mwamuzi mwenye haki,

Mungu aghadhibikaye kila siku.

7:12 Eze 3:19; 33:9; Kum 32:4; Za 21:12; 2Sam 22:35; Isa 5:28; 13:18Kama hakutuhurumia,

atanoa upanga wake,

ataupinda na kuufunga uzi upinde wake.

7:13 Za 11:2; 18:14; 64:3Ameandaa silaha zake kali,

ameweka tayari mishale yake ya moto.

7:14 Isa 59:4; Yak 1:15Yeye aliye na mimba ya uovu

na achukuaye mimba ya ghasia huzaa uongo.

7:15 Za 35:7, 8; 40:2; 94:13; Mit 26:27; Ay 4:8; Es 7:10; Mit 5:22Yeye achimbaye shimo na kulifukua

hutumbukia katika shimo alilochimba mwenyewe.

7:16 1Fal 2:23Ghasia azianzishazo humrudia mwenyewe,

ukatili wake humrudia kichwani.

7:17 2Nya 31:2; Za 5:8; Rum 15:11; Mwa 14:18; Ebr 2:12Nitamshukuru Bwana kwa ajili ya haki yake,

na nitaliimbia sifa jina la Bwana Aliye Juu Sana.

Read More of Zaburi 7