Zaburi 7:1-9 NEN

Zaburi 7:1-9

Zaburi 7

Sala Ya Mtu Anayedhulumiwa

Ombolezo la Daudi kwa Bwana kwa sababu ya Kushi, Mbenyamini.

7:1 Za 2:12; 11:1; 31:1; 3:7; 31:15; 119:86, 157, 161Ee Bwana, Mungu wangu, ninakukimbilia wewe,

uniokoe na kunikomboa na wote wanaonifuatia,

7:2 Mwa 49:9; Ufu 4:7; Za 3:2; 71:11; 1Pet 5:8la sivyo watanirarua kama simba

na kunichana vipande vipande, asiwepo wa kuniokoa.

7:3 Za 35:7, 19; Mit 24:28; 1Sam 24:7Ee Bwana, Mungu wangu, kama nimetenda haya

na kuna hatia mikononi mwangu,

7:4 Za 35:7, 19; Mit 24:28; 1Sam 24:7au ikiwa nimemtenda uovu aliye na amani nami,

au nimemnyangʼanya adui yangu pasipo sababu,

7:5 Kut 15:9; Ay 7:21; 2Sam 22:43; 2Fal 9:33; Isa 10:6; Mao 3:16basi adui anifuatie na kunipata,

auponde uhai wangu ardhini

na kunilaza mavumbini.

7:6 2Nya 6:41; Za 138:7; 35:23; 44:23; 94:2Amka kwa hasira yako, Ee Bwana,

inuka dhidi ya ghadhabu ya adui zangu.

Amka, Mungu wangu, uamue haki.

7:7 Za 68:18Kusanyiko la watu na likuzunguke.

Watawale kutoka juu.

7:8 1Nya 16:33; Mk 5:7; 1Sam 26:23; Za 18:20; Mwa 3:5; 20:5; Hes 24:16Bwana na awahukumu kabila za watu.

Nihukumu Ee Bwana,

kwa kadiri ya haki yangu,

kwa kadiri ya uadilifu wangu,

Ewe Uliye Juu Sana.

7:9 Yer 11:20; Ufu 2:23; Za 26:2; 37:23; 40:2; 1Sam 16:7; 1Nya 28:9Ee Mungu mwenye haki,

uchunguzaye mawazo na mioyo,

komesha ghasia za waovu

na ufanye wenye haki waishi kwa amani.

Read More of Zaburi 7