Zaburi 69:29-36 NEN

Zaburi 69:29-36

69:29 Za 20:1Mimi niko katika maumivu na dhiki;

Ee Mungu, wokovu wako na unihifadhi.

69:30 Za 28:7; 34:3Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,

nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani.

69:31 Za 50:9-13; 51:16Hili litampendeza Bwana kuliko ngʼombe dume,

zaidi ya fahali akiwa na pembe na kwato zake.

69:32 Za 34:2; 22:26Maskini wataona na kufurahi:

ninyi mnaomtafuta Mungu, mioyo yenu na iishi!

69:33 Za 12:5Bwana huwasikia wahitaji

wala hadharau watu wake waliotekwa.

69:34 Za 96:11; 98:7; Isa 44:23Mbingu na dunia zimsifu,

bahari na vyote viendavyo ndani yake,

69:35 Oba 1:17; Ezr 9:9; Za 51:18kwa maana Mungu ataiokoa Sayuni

na kuijenga tena miji ya Yuda.

Kisha watu watafanya makao yao humo na kuimiliki,

69:36 Za 25:13; 37:29watoto wa watumishi wake watairithi

na wale wote walipendao jina lake

wataishi humo.

Read More of Zaburi 69