Zaburi 69:13-28 NEN

Zaburi 69:13-28

69:13 Isa 49:8; 2Kor 6:2; Za 17:7; 51:1Lakini Ee Bwana, ninakuomba,

kwa wakati ukupendezao;

katika upendo wako mkuu, Ee Mungu,

unijibu kwa wokovu wako wa hakika.

69:14 Za 69:2; 144:7Uniokoe katika matope,

usiniache nizame;

niokoe na hao wanichukiao,

kutoka kwenye vilindi vya maji.

69:15 Za 36:6; 68:22; Hes 21:33; Yer 22:2069:15 Za 28:1; 124:4, 5; Hes 16:33Usiache mafuriko yanigharikishe

au vilindi vinimeze,

au shimo lifumbe kinywa chake juu yangu.

69:16 Za 63:3Ee Bwana, unijibu, kwa wema wa upendo wako;

kwa huruma zako nyingi unigeukie.

69:17 Za 22:24; 143:7; 50:15; 66:14Usimfiche mtumishi wako uso wako,

uharakishe kunijibu, kwa sababu niko katika shida.

69:18 Za 49:15Njoo karibu uniokoe,

nikomboe kwa sababu ya adui zangu.

69:19 Za 22:6Unajua jinsi ninavyodharauliwa,

kufedheheshwa na kuaibishwa,

adui zangu wote unawajua.

69:20 Ay 16:2; Isa 63:5; Za 142:4Dharau zimenivunja moyo

na nimekata tamaa,

nimetafuta wa kunihurumia, lakini sikumpata,

wa kunituliza, lakini sikumpata.

69:21 Hes 6:3; Lk 23:36; Mt 27:34, 48; Mk 15:23, 36; Yn 19:28-30Waliweka nyongo katika chakula changu

na walinipa siki nilipokuwa na kiu.

69:22 1Sam 28:9; Ay 18:10Meza iliyoandaliwa mbele yao na iwe mtego,

nayo iwe upatilizo na tanzi.

69:23 Rum 11:9-10Macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona,

nayo migongo yao iinamishwe daima.

69:24 Za 79:6; Yer 10:25Uwamwagie ghadhabu yako,

hasira yako kali na iwapate.

69:25 Law 26:43; Mt 23:38; Mdo 1:20Mahali pao na pawe ukiwa,

wala asiwepo yeyote atakayeishi katika mahema yao.

69:26 Ay 19:22; Zek 1:15Kwa kuwa wanawatesa wale uliowajeruhi,

na kuzungumza juu ya maumivu ya wale uliowaumiza.

69:27 Neh 4:5; Za 109:14Walipize uovu juu ya uovu,

usiwaache washiriki katika wokovu wako.

69:28 Kut 32:32-33; Lk 10:20; Eze 13:9Wafutwe kutoka kitabu cha uzima

na wasiorodheshwe pamoja na wenye haki.

Read More of Zaburi 69