Zaburi 69:1-12
Zaburi 69
Kilio Cha Kuomba Msaada Wakati Wa Dhiki
Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Yungiyungi.” Zaburi ya Daudi.
69:1 Za 42:7; 32:6; Yon 2:5Ee Mungu, niokoe,
kwa maana maji yamenifika shingoni.
69:2 Ay 30:19Ninazama kwenye vilindi vya matope,
pasipo mahali pa kukanyaga,
Nimefika kwenye maji makuu,
mafuriko yamenigharikisha.
69:3 Za 6:6; 119:82Nimechoka kwa kuomba msaada,
koo langu limekauka.
Macho yangu yanafifia,
nikimtafuta Mungu wangu.
69:4 Yn 15:25; Za 25:19; 35:19; 38:19; 40:14; 119:95; Isa 32:7Wale wanaonichukia bila sababu
ni wengi kuliko nywele za kichwa changu;
wengi ni adui kwangu bila sababu,
wale wanaotafuta kuniangamiza.
Ninalazimishwa kurudisha
kitu ambacho sikuiba.
69:5 Za 38:5; 44:21Ee Mungu, wewe unajua upumbavu wangu,
wala hatia yangu haikufichika kwako.
Ee Bwana, ewe Bwana Mwenye Nguvu Zote,
wakutumainio wasiaibishwe
kwa ajili yangu;
wakutafutao wasifedheheshwe kwa ajili yangu,
Ee Mungu wa Israeli.
69:7 Yer 15:15; Za 39:8; 44:15Kwa maana nimestahimili dharau kwa ajili yako,
aibu imefunika uso wangu.
69:8 Ay 19:13-15; Za 31:11; 38:11; Isa 53:3; Yn 7:5Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu,
mgeni kwa wana wa mama yangu mwenyewe.
69:9 Yn 2:17; Rum 15:3; Za 89:50-51Kwa kuwa wivu wa nyumba yako unanila,
matukano ya wale wanaokutukana yameniangukia.
69:10 Za 35:13Ninapolia na kufunga,
lazima nivumilie matusi.
69:11 2Sam 3:31; Za 35:13Ninapovaa nguo ya gunia,
watu hunidharau.
69:12 Mwa 18:1; 23:10; Ay 30:9Wale wanaoketi mlangoni wananisimanga,
nimekuwa wimbo wa walevi.