Zaburi 68:7-14
68:7 Kut 13:21; Za 78:40; 106:14Ee Mungu, ulipowatangulia watu wako,
ulipopita nyikani,
68:8 2Sam 22:8; Amu 5:4, 5; Mhu 11:3; 2Sam 21:10; Kum 33:2dunia ilitikisika,
mbingu zikanyesha mvua,
mbele za Mungu, Yule wa Sinai,
mbele za Mungu, Mungu wa Israeli.
68:9 Kum 32:2; Ay 36:28; Eze 34:26Ee Mungu, ulinyesha mvua nyingi
na kuiburudisha ardhi iliyokuwa imechoka.
68:10 Kum 28:12; Za 65:9Ee Mungu, watu wako waliishi huko,
nawe kwa wingi wa utajiri wako
uliwapa maskini mahitaji yao.
68:11 Lk 2:13Bwana alitangaza neno,
waliolitangaza neno hilo walikuwa kundi kubwa:
68:12 Yos 10:16; Amu 5:30“Wafalme na majeshi walikimbia upesi,
watu waliobaki kambini waligawana nyara.
68:13 Mwa 49:14Hata ulalapo katikati ya mioto ya kambini,
mabawa ya njiwa wangu yamefunikwa kwa fedha,
manyoya yake kwa dhahabu ingʼaayo.”
68:14 2Sam 22:15; Amu 9:48Wakati Mwenyezi68:14 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania. alipowatawanya wafalme katika nchi,
ilikuwa kama theluji iliyoanguka juu ya Salmoni.