Zaburi 68:15-20 NEN

Zaburi 68:15-20

Milima ya Bashani ni milima iliyotukuka,

milima ya Bashani ina vilele vilivyochongoka.

68:16 Za 132:13, 14; 2:6; Kum 12:5Enyi milima yenye vilele vilivyochongoka,

kwa nini mnakazia macho kwa wivu,

katika mlima Mungu anaochagua kutawala,

ambako Bwana mwenyewe ataishi milele?

68:17 2Fal 2:11; Isa 66:15; Hab 3:8; Dan 7:10Magari ya Mungu ni makumi ya maelfu,

na maelfu ya maelfu;

Bwana amekuja kutoka Sinai

hadi katika patakatifu pake.

68:18 Za 47:5; 7:7; Amu 5:12; Efe 4:8; Hes 17:10Ulipopanda juu, uliteka mateka,

ukapokea vipawa kutoka kwa wanadamu,

hata kutoka kwa wale walioasi,

ili wewe, Ee Bwana Mungu, upate kuishi huko.

68:19 Za 65:5; 81:6Sifa apewe Bwana, Mungu Mwokozi wetu,

ambaye siku kwa siku hutuchukulia mizigo yetu.

68:20 1Sam 10:19; Za 56:13; Yer 45; 5; Eze 6:8Mungu wetu ni Mungu aokoaye,

Bwana Mwenyezi hutuokoa na kifo.

Read More of Zaburi 68