Zaburi 68:1-6
Zaburi 68
Wimbo Wa Taifa Wa Shangwe Kwa Ushindi
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi. Wimbo.
68:1 Za 89:10; 132:8; 12:5; 18:14; 92:9; 144:6; Hes 10:35; Isa 17:13; 21:15; 33:3Mungu na ainuke, watesi wake watawanyike,
adui zake na wakimbie mbele zake.
68:2 Za 37:20; 80:16; 22:14; 9:3; Hes 10:35Kama vile moshi upeperushwavyo na upepo,
vivyo hivyo uwapeperushe mbali,
kama vile nta iyeyukavyo kwenye moto,
vivyo hivyo waovu na waangamie mbele za Mungu.
68:3 Za 64:10; 97:12Bali wenye haki na wafurahi,
washangilie mbele za Mungu,
wafurahi na kushangilia.
68:4 2Sam 22:50; Za 7:17; 30:4; 66:2; 68:33; 96:2; 100:4; 135:3; 83:18; Kut 6:3; 20:21; Kum 33:26Mwimbieni Mungu, liimbieni sifa jina lake,
mtukuzeni yeye aendeshwaye juu ya mawingu:
jina lake ni Bwana,
furahini mbele zake.
68:5 Za 10:14; Kut 22:22; Kum 10:18; 26:15; Yer 25:30Baba wa yatima, mtetezi wa wajane,
ni Mungu katika makao yake matakatifu.
68:6 Lk 4:18; Za 146:7; 113:9; 102:20; 79:11; 25:16; Isa 58:11; 35:7; 49:10; 61:1Mungu huwaweka wapweke katika jamaa,
huwaongoza wafungwa wakiimba,
bali waasi huishi katika nchi kame.