Zaburi 67:1-7 NEN

Zaburi 67:1-7

Zaburi 67

Mataifa Yahimizwa Kumsifu Mungu

Kwa mwimbishaji. Na ala za nyuzi za muziki. Zaburi. Wimbo.

67:1 Hes 6:24-26; Za 4:6; 31:16; 119:135; 2Kor 4:6Mungu aturehemu na kutubariki,

na kutuangazia nuru za uso wake,

67:2 Isa 40:5; 52:10; 62:1, 2; Lk 2:30-32; Tit 2:11; Za 98:2; Mdo 10:35; 13:10ili njia zako zijulikane duniani,

wokovu wako katikati ya mataifa yote.

67:3 Za 67:5; Isa 24:15, 16Ee Mungu, mataifa na wakusifu,

mataifa yote na wakusifu.

67:4 Za 100:1-2; 9:4; 96:10-13; 68:32Mataifa yote wafurahi na kuimba kwa shangwe,

kwa kuwa unatawala watu kwa haki

na kuongoza mataifa ya dunia.

67:5 Za 67:3Ee Mungu, mataifa na wakusifu,

mataifa yote na wakusifu.

67:6 Mwa 8:22; 12:2; Law 26:4; Za 85:12; Isa 55:10; Eze 34:27; Zek 8:12Ndipo nchi itatoa mazao yake,

naye Mungu, Mungu wetu, atatubariki.

67:7 Za 2:8; 33:8Mungu atatubariki

na miisho yote ya dunia itamcha yeye.

Read More of Zaburi 67