Zaburi 66:13-20 NEN

Zaburi 66:13-20

66:13 Za 51:19; 22:25; 50:14; 116:14; Mhu 5:4; Yon 2:9Nitakuja hekaluni mwako na sadaka za kuteketezwa

na kukutimizia nadhiri zangu:

nadhiri ambazo midomo yangu iliahidi

na nilizotamka kwa kinywa changu

nilipokuwa katika shida.

66:15 Law 16:5; Za 51:19Nitakutolea dhabihu za wanyama wanono

na sadaka za kondoo dume,

nitakutolea mafahali na mbuzi.

66:16 Za 34:11; 71:15, 24Njooni msikilize ninyi nyote mnaomcha Mungu,

nami niwaambie aliyonitendea.

Nilimlilia kwa kinywa changu,

sifa zake zilikuwa katika ulimi wangu.

66:18 Kum 1:45; 1Sam 8:18; Yak 4:3; Isa 1:15; Ay 11:14, 15; Mit 15:29Kama ningekuwa nimeyaficha maovu moyoni mwangu,

Bwana asingekuwa amenisikiliza;

66:19 Za 18:6lakini hakika Mungu amenisikiliza

na amesikia sauti yangu katika maombi.

66:20 Za 22:24Sifa apewe Mungu,

ambaye hakulikataa ombi langu

wala kunizuilia upendo wake!

Read More of Zaburi 66