Zaburi 66:1-12
Zaburi 66
Kusifu Mungu Kwa Ajili Ya Wema Wake
Kwa mwimbishaji. Wimbo. Zaburi.
66:1 Za 81:1; 84:8; 98:4; 100:1Mpigieni Mungu kelele za shangwe, dunia yote!
66:2 Za 79:9; 86:9; Isa 42:8, 12; 43:21Imbeni utukufu wa jina lake;
mpeni sifa zake kwa utukufu!
66:3 Kum 7:21; 10:21; Za 106:22; 111:6; 18:44; 65:5; 145:6; 2Sam 22:45Mwambieni Mungu, “Jinsi gani yalivyo ya kutisha matendo yako!
Uwezo wako ni mkuu mno kiasi kwamba
adui wananyenyekea mbele zako.
66:4 Za 22:27; 7:17; 67:3Dunia yote yakusujudia,
wanakuimbia wewe sifa,
wanaliimbia sifa jina lako.”
66:5 Za 66:3; 46:8; 106:22Njooni mwone yale Mungu aliyoyatenda,
mambo ya kutisha aliyoyatenda
miongoni mwa wanadamu!
66:6 Mwa 8:1; Kut 14:21, 22; Law 23:40; Yos 3:14; Za 78:13; Isa 63:13, 14; 1Kor 10:1Alifanya bahari kuwa nchi kavu,
wakapita kati ya maji kwa miguu,
njooni, tumshangilie.
66:7 Kut 15:18; 3:16; Hes 17:10; Za 11:4; 112:10; 140:8; 145:13Yeye hutawala kwa uwezo wake milele,
macho yake huangalia mataifa yote:
waasi wasithubutu kujiinua dhidi yake.
66:8 Za 22:23Enyi mataifa, msifuni Mungu wetu,
sauti ya sifa yake isikike,
66:9 Za 30:3; Kum 32:35; Ay 12:5ameyahifadhi maisha yetu
na kuizuia miguu yetu kuteleza.
66:10 Kut 15:25; Ay 6:29; 28:1; Za 12:6; Zek 13:9Ee Mungu, wewe ulitujaribu,
ukatusafisha kama fedha.
66:11 Za 38:4; 142:7; 146:7; Isa 61:1; 10:27; 42:7, 22; Mwa 3:17; Kut 1:14Umetuingiza kwenye nyavu
na umetubebesha mizigo mizito
migongoni mwetu.
66:12 Isa 51:13; Za 18:19Uliwaruhusu watu watukalie vichwani,
tulipita kwenye moto na kwenye maji,
lakini ulituleta kwenye nchi
iliyojaa utajiri tele.