Zaburi 60:1-4 NEN

Zaburi 60:1-4

Zaburi 60

Kuomba Kuokolewa

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Shushani Eduthi.” Utenzi wa Daudi wa kufundisha. Wakati alipopigana na Waaramu kutoka Aramu-Naharaimu na Aramu-Soba, naye Yoabu akarudi nyuma na kuwaua Waedomu 12,000 katika Bonde la Chumvi.

60:1 2Sam 5:20; Za 18:7; 44:9; 79:5; 80:3; 60:2; 2Nya 7:14Ee Mungu, umetukataa na kutokea ghafula juu yetu,

umekasirika: sasa turejeshe upya!

Umetetemesha nchi na kuipasua;

uiponye mavunjiko yake, kwa maana inatetemeka.

60:3 Za 71:20; 75:8; Isa 29:9; 51:17; 63:6; Yer 25:16; Zek 12:2; Ufu 14:10Umewaonyesha watu wako nyakati za kukata tamaa;

umetunywesha mvinyo unaotuyumbisha.

60:4 Isa 5:26; 11:10, 12; 18:3Kwa wale wanaokucha wewe,

umewainulia bendera,

ili iweze kutwekwa dhidi ya upinde.

Read More of Zaburi 60