Zaburi 59:9-17 NEN

Zaburi 59:9-17

59:9 Za 18:1; 9:9; 18:2; 62:2; 71:3Ee nguvu yangu, ninakutazama wewe,

wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu,

Mungu wangu unipendaye.

Mungu atanitangulia,

naye atanifanya niwachekelee

wale wanaonisingizia.

59:11 Kum 4:9; 6:12; Za 3:3; 84:9; 89:10; 106:27; 144:6; Isa 33:3; Mwa 4:12, 13Lakini usiwaue, Ee Bwana, ngao yetu,

au sivyo watu wangu watasahau.

Katika uwezo wako wafanye watangetange

na uwashushe chini.

59:12 Za 10:7; 64:8; Mit 10:14; 12:13; Isa 2:12; 5:15; Sef 3:11Kwa ajili ya dhambi za vinywa vyao,

kwa ajili ya maneno ya midomo yao,

waache wanaswe katika kiburi chao.

Kwa ajili ya laana na uongo wanaotamka,

59:13 Za 83:18; 104:35wateketeze katika ghadhabu,

wateketeze hadi wasiwepo tena.

Ndipo itakapofahamika katika miisho ya dunia

kwamba Mungu anatawala juu ya Yakobo.

Hurudi jioni,

wakibweka kama mbwa,

wakiuzurura mji.

59:15 Ay 15:23Wanatangatanga wakitafuta chakula,

wasipotosheka hubweka kama mbwa.

59:16 Za 5:3; 88:13; 101:1; 108:1; 1Sam 2:10; 2Sam 22:3; Kum 4:30Lakini mimi nitaziimba nguvu zako,

asubuhi nitaimba juu ya upendo wako;

kwa maana wewe ndiwe ngome yangu

na kimbilio langu wakati wa shida.

59:17 Za 59:1Ee uliye Nguvu zangu, ninakuimbia sifa.

Wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu,

Mungu unipendaye.

Read More of Zaburi 59