Zaburi 58:1-11 NEN

Zaburi 58:1-11

Zaburi 58

Mungu Kuwaadhibu Waovu

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa “Usiharibu!” Utenzi wa Daudi.

Enyi watawala, je, kweli mwanena kwa haki?

Je, mnahukumu kwa unyofu miongoni mwa watu?

58:2 Za 74:20; Isa 10:1; Mt 15:19; Lk 6:38La, mioyoni mwenu mnatunga udhalimu,

na mikono yenu hupima jeuri duniani.

58:3 Za 51:5Waovu ni wapotovu tangu kuzaliwa kwao,

toka tumboni mwa mama zao

ni wakaidi na husema uongo.

58:4 Hes 21:6; Za 140:4Sumu yao ni kama sumu ya nyoka,

kama ile ya fira ambaye ameziba masikio yake,

58:5 Za 81:11; Mhu 10:1; Yer 8:17ambaye hatasikia sauti ya kutumbuiza ya mwaguzi,

hata kama mganga angecheza kwa ustadi kiasi gani.

58:6 Ay 4:10; Za 3:7Ee Mungu, yavunje meno katika vinywa vyao;

Ee Bwana, vunja meno makali ya hao simba!

58:7 Law 26:36; Ay 11:16; Za 11:2; 57:4; 64:3Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi,

wavutapo pinde zao, mishale yao na iwe butu.

58:8 Isa 13:7; Ay 3:16Kama konokono ayeyukavyo akitembea,

kama mtoto aliyezaliwa akiwa mfu,

wasilione jua.

58:9 Za 118:12; Mhu 7:6; Ay 7:10; Mit 10:25Kabla vyungu vyenu havijapata moto wa kuni za miiba,

zikiwa mbichi au kavu,

waovu watakuwa

wamefagiliwa mbali.

58:10 Ay 22:19; Kum 32:42; 32:35; Yer 11:20; Mit 10:11; Rum 12:17-21; Za 18:47; 7:9; 91:8; 68:23; Ufu 18:20Wenye haki watafurahi waonapo wakilipizwa kisasi,

watakapochovya nyayo zao katika damu ya waovu.

58:11 Mwa 4:12, 13; 15:1; Za 128:2; Lk 6:23; Ufu 2:23; Rum 2:6-11; 14:12; Ay 34:11; Mhu 5:8; Yer 32:19; Eze 7:27Ndipo wanadamu watasema,

“Hakika utulivu wa wenye haki bado una thawabu,

hakika kuna Mungu ahukumuye dunia.”

Read More of Zaburi 58