Zaburi 57:7-11 NEN

Zaburi 57:7-11

57:7 Za 112:7; 108:1Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti;

nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.

57:8 Za 33:2; 149:3; 150:3; Amu 5:12Amka, nafsi yangu!

Amka, kinubi na zeze!

Nitayaamsha mapambazuko.

Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa;

nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu.

57:10 Za 36:5; 108:4Kwa maana upendo wako ni mkuu, waenea hadi mbinguni,

uaminifu wako unazifikia anga.

57:11 Za 8:1; 149:3; 150:3; Amu 5:12Ee Mungu, utukuzwe juu mbinguni,

utukufu wako na uwe duniani pote.

Read More of Zaburi 57