Zaburi 55:1-11
Zaburi 55
Maombi Ya Mtu Aliyesalitiwa Na Rafiki
Kwa mwimbishaji. Na ala za uimbaji. Utenzi wa Daudi.
55:1 Za 27:9; Mao 3:56Ee Mungu, sikiliza maombi yangu,
wala usidharau hoja yangu.
55:2 1Sam 1:15-16; Za 4:1; 77:3; 86:6-7; 142:2Nisikie na unijibu.
Mawazo yangu yananisumbua na nimehangaishwa
55:3 2Sam 16:6-8; 17:9; Za 143:3; 44:16; 71:11kwa sauti ya adui,
kwa kukaziwa macho na waovu,
kwa sababu wananiletea mateso juu yangu
na kunitukana kwa hasira zao.
55:4 Ay 18:11; Za 6:3; 102:3-5; Yn 12:27; Mt 26:37, 38; 2Kor 1:8-10Moyo wangu umejaa uchungu,
hofu ya kifo imenishambulia.
55:5 Ay 4:14; Eze 7:18; 2Kor 7:15; Isa 21:4; Kum 28:67; Yer 46:5; 49:5Woga na kutetemeka vimenizunguka,
hofu kuu imenigharikisha.
Nilisema, “Laiti ningekuwa na mbawa za njiwa!
Ningeruka niende mbali kupumzika.
55:7 1Sam 23:14Ningalitorokea mbali sana
na kukaa jangwani,
55:8 Za 31:20; 77:18; Isa 4:6; 25:4; 28:2; 29:6; 32:2ningaliharakisha kwenda mahali pa salama,
mbali na tufani kali na dhoruba.”
55:9 Mwa 4:17; 11:9; Mdo 2:4; Za 11:5; Isa 59:6; Yer 6:7; Eze 7:11; Hab 1:3Ee Bwana, uwatahayarishe waovu
na uwachanganyishie semi zao,
maana nimeona jeuri na ugomvi mjini.
55:10 1Pet 5:8Usiku na mchana wanazunguka juu ya kuta zake,
uovu na dhuluma vimo ndani yake.
55:11 Za 5:9; 10:7Nguvu za uharibifu zinatenda kazi mjini,
vitisho na uongo haviondoki mitaani mwake.