Zaburi 51:10-19 NEN

Zaburi 51:10-19

51:10 Za 24:4; 78:37; Mt 5:8; Mdo 15:9; Eze 11:19; 18:31; 36:26; Mit 20:9; Yer 13:27; Efe 2:10Ee Mungu, uniumbie moyo safi,

uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.

51:11 Za 27:9; 138:8; 71:9; 106:3; Kut 33:15; Mwa 4:14; Isa 63:10; Eze 36:27; Efe 4:30; Rum 8:9Usinitupe kutoka mbele zako

wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu.

51:12 Ay 33:26; Za 110:3; 18:35; Rum 8:15; 2Kor 3:17Unirudishie tena furaha ya wokovu wako,

unipe roho ya utii, ili initegemeze.

51:13 Kut 33:13; Za 1:1; Mdo 9:21-22; Ay 33:27Ndipo nitakapowafundisha wakosaji njia zako,

na wenye dhambi watakugeukia wewe.

51:14 2Sam 12:9; Za 5:8; 22:5; 39:8; 68:20; 88:1; 35:28; 71:15Ee Mungu, Mungu uniokoaye,

niokoe na hatia ya kumwaga damu,

nao ulimi wangu utaimba juu ya haki yako.

51:15 Kut 4:15Ee Bwana, fungua midomo yangu,

na kinywa changu kitatangaza sifa zako.

51:16 1Sam 15:22Wewe hupendezwi na dhabihu, au ningaliileta,

hufurahii sadaka za kuteketezwa.

51:17 Mit 15:8; Hag 2:14; Mt 11:29Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika,

moyo uliovunjika wenye toba,

Ee Mungu, hutaudharau.

51:18 Za 69:35; 147:2; 102:16; Zek 1:16-17; Isa 14:32; 44:26; 51:3; 51:19; Kum 33:19; Mal 3:3Kwa wema wa radhi yako uifanye Sayuni istawi,

ukazijenge upya kuta za Yerusalemu.

Hapo ndipo kutakapokuwa na dhabihu za haki,

sadaka nzima za kuteketezwa za kukupendeza sana,

pia mafahali watatolewa

madhabahuni mwako.

Read More of Zaburi 51