Zaburi 48:1-8 NEN

Zaburi 48:1-8

Zaburi 48

Sayuni, Mji Wa Mungu

Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora.

48:1 2Sam 22:4; Mik 4:1; Yer 10:6; 31:23; Za 86:10; 96:4; 99:2; 135:5; 147:5; 46:4; 87:1; 18:3; 2:6; 1Nya 16:25; Kum 33:19; Isa 2:2; 11:9; 32:16; Zek 8:3; Oba 1:17; Dan 9:16Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana,

katika mji wa Mungu wetu,

mlima wake mtakatifu.

48:2 Isa 14:13; Za 2:6; 50:2; Mao 2:15; Eze 16:14; 20:6; Yos 13:17; Mt 5:35; Yer 3:19Ni mzuri katika kuinuka kwake juu sana,

furaha ya dunia yote.

Kama vilele vya juu sana vya Safoni48:2 Safoni inaweza ikawa na maana ya mlima mtakatifu au upande wa kaskazini. ni Mlima Sayuni,

mji wa Mfalme Mkuu.

48:3 Za 122:7; 18:2Mungu yuko katika ngome zake;

amejionyesha mwenyewe kuwa ngome yake.

48:4 2Sam 10:1-19Wakati wafalme walipounganisha nguvu,

waliposonga mbele pamoja,

48:5 Kut 15:16walimwona nao wakashangaa,

wakakimbia kwa hofu.

48:6 Ay 4:14; Mwa 3:16Kutetemeka kuliwashika huko,

maumivu kama ya mwanamke

mwenye utungu wa kuzaa.

48:7 Mwa 10:4; 41:6; 1Fal 10:22; 22:48; Eze 27:26Uliwaangamiza kama meli za Tarshishi

zilizovunjwa na upepo wa mashariki.

48:8 Yer 23:6; Mik 4:1; Zek 8:13; 14:11; Isa 2:2Kama tulivyokuwa tumesikia,

ndivyo tulivyoona

katika mji wa Bwana Mwenye Nguvu Zote,

katika mji wa Mungu wetu:

Mungu ataufanya uwe salama milele.

Read More of Zaburi 48