Zaburi 45:1-9 NEN

Zaburi 45:1-9

Zaburi 45

Wimbo Wa Arusi Ya Kifalme

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa utenzi wa “Yungiyungi.” Utenzi wa wana wa Kora. Wimbo wa arusi.

Moyo wangu umesisimuliwa na jambo jema

ninapomsimulia mfalme mabeti yangu;

ulimi wangu ni kalamu ya mwandishi stadi.

45:2 Lk 4:22; Za 21:6Wewe ni bora kuliko watu wengine wote

na midomo yako imepakwa neema,

kwa kuwa Mungu amekubariki milele.

45:3 Kum 32:41; Ufu 1:16; Za 21:5; 149:6; 2Sam 1:19; Ay 40:10Jifunge upanga wako pajani mwako, ee mwenye nguvu,

jivike fahari na utukufu.

45:4 Ufu 6:2; Sef 2:3; Za 21:8; 65:5; 66:3; Kum 4:34Katika fahari yako, songa mbele kwa ushindi,

kwa ajili ya kweli, unyenyekevu na haki,

mkono wako wa kuume na uonyeshe matendo ya kutisha.

45:5 Kum 32:23; Hes 24:8; Isa 50:10; Za 56:3, 11; 9:13; 92:9; Mao 3:24Mishale yako mikali na ichome mioyo ya adui za mfalme,

mataifa na yaanguke chini ya nyayo zako.

45:6 Mwa 21:33; Mao 5:13; Za 93:2; Isa 9:6, 7; Ebr 1:8Ee Mungu, kiti chako cha enzi

kitadumu milele na milele,

fimbo ya utawala wa haki

itakuwa fimbo ya utawala wa ufalme wako.

45:7 Za 33:5; 11:5; 2:2; 23:5; Ebr 1:9; Eze 7:26; Isa 45:1; 61:1; Yn 20:17; Mt 3:15; Zek 4:14Unaipenda haki na kuchukia uovu;

kwa hiyo Mungu, Mungu wako,

amekuweka juu ya wenzako,

kwa kukupaka mafuta ya furaha.

45:8 Kum 28:8; Wim 1:3; 4:10; Mwa 37:25; Hes 24:6; Yn 19:39; Kut 30:24; 1Fal 22:39; Za 144:9; 150:4; Isa 38:20; Mt 27:9Mavazi yako yote yana harufu nzuri

ya manemane, udi na mdalasini;

kutoka kwenye majumba ya kifalme

yaliyopambwa kwa pembe za ndovu,

sauti za vinanda vya nyuzi

zinakufanya ufurahi.

45:9 Wim 6:8; Isa 62:5; Mwa 10:29; 1Fal 2:19Binti za wafalme ni miongoni mwa wanawake wako waheshimiwa;

kuume kwako yupo bibi arusi malkia aliyevaa dhahabu ya Ofiri.

Read More of Zaburi 45