Zaburi 42:7-11 NEN

Zaburi 42:7-11

42:7 Eze 7:26; Mwa 1:2; 7:11; Za 69:2; Yon 2:3Kilindi huita kilindi,

katika ngurumo za maporomoko ya maji yako;

mawimbi yako yote pamoja na viwimbi

vimepita juu yangu.

42:8 Za 57:3; 16:7; 133:3; Mhu 5:18; 8:15; Kum 28:8Mchana Bwana huelekeza upendo wake,

usiku wimbo wake uko nami:

maombi kwa Mungu wa uzima wangu.

42:9 Za 18:31; 10:11; 35:14; 106:42; 9:13; 43:2; Ay 20:19Ninamwambia Mungu Mwamba wangu,

“Kwa nini umenisahau?

Kwa nini niendelee kuomboleza,

nikiwa nimeonewa na adui?”

42:10 Za 89:51; 119:42; 44:16; 6:2; 102:8; Kum 32:27Mifupa yangu inateseka kwa maumivu makali

adui zangu wanaponidhihaki,

wakiniambia mchana kutwa,

“Yuko wapi Mungu wako?”

42:11 Za 43:5Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka?

Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?

Weka tumaini lako kwa Mungu,

kwa sababu bado nitamsifu,

Mwokozi wangu na Mungu wangu.

Read More of Zaburi 42