Zaburi 41:7-13 NEN

Zaburi 41:7-13

41:7 Za 71:10Adui zangu wote hunongʼonezana dhidi yangu,

hao huniwazia mabaya sana, wakisema,

41:8 2Fal 1:4“Ugonjwa mbaya sana umempata,

kamwe hatainuka tena kitandani mwake.”

41:9 Oba 1:7; Yn 13:18; 2Sam 15:12; Ay 19:14, 19; Hes 30:2; Lk 22:21; Za 55:20; 89:34; Mt 26:23Hata rafiki yangu wa karibu niliyemwamini,

yule aliyekula chakula changu

ameniinulia kisigino chake.

41:10 Za 3:3; 9:13; 2Sam 3:39Lakini wewe, Ee Bwana, nihurumie,

ukaniinue tena, ili niweze kuwalipiza kisasi.

41:11 Hes 14:8; Za 25:2Najua kwamba wapendezwa nami,

kwa kuwa adui yangu hanishindi.

41:12 Za 21:6; 61:7; 34:15; 25:21; 18:35; 37:17; 63:8; Ay 4:7; Mdo 2:38Katika uadilifu wangu unanitegemeza

na kuniweka kwenye uwepo wako milele.

41:13 Mwa 24:27; Za 72:18, 19; 89:52; 106:48Msifuni Bwana, Mungu wa Israeli,

tangu milele na hata milele.

Amen na Amen.

Read More of Zaburi 41