Zaburi 40:9-17 NEN

Zaburi 40:9-17

40:9 Za 22:25, 31; 139:2; Yos 22:22Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa,

sikufunga mdomo wangu,

Ee Bwana, kama ujuavyo.

40:10 Za 89:1; 22:22; Mdo 20:20; Flp 3:9; Rum 1:16, 17Sikuficha haki yako moyoni mwangu;

ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako.

Sikuficha upendo wako na kweli yako

mbele ya kusanyiko kubwa.

40:11 Zek 1:12; Za 26:3; 61:7; 43:3; Mit 20:28Ee Bwana, usizuilie huruma zako,

upendo wako na kweli yako daima vinilinde.

40:12 Za 25:17; 38:4; 65:3; 69:4; 73:26Kwa maana taabu zisizo na hesabu zimenizunguka,

dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona.

Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu,

nao moyo unazimia ndani yangu.

40:13 Za 22:19; 38:22Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa;

Ee Bwana, njoo hima unisaidie.

40:14 1Sam 20:1; Es 9:2; Za 35:26; 35:4Wote wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,

waaibishwe na kufadhaishwa;

wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,

warudishwe nyuma kwa aibu.

40:15 Za 35:21Wale waniambiao, “Aha! Aha!”

wafadhaishwe na iwe aibu yao.

40:16 Kum 4:29; 1Nya 28:9; Za 9:10; 119:2; 9:2; 35:27Lakini wote wakutafutao

washangilie na kukufurahia,

wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,

Bwana atukuzwe!”

40:17 Neh 5:19; Mk 10:21; Za 86:1; 109:22; 144:3; 20:2; 18:2; 119:60Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji;

Bwana na anifikirie.

Wewe ndiwe msaada wangu na Mwokozi wangu;

Ee Mungu wangu, usikawie.

Read More of Zaburi 40