Zaburi 38:1-11 NEN

Zaburi 38:1-11

Zaburi 38

Maombi Ya Mtu Anayeteseka

Zaburi ya Daudi. Maombi.

38:1 Za 6:1Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako,

wala kuniadhibu katika ghadhabu yako.

38:2 Ay 6:4Kwa kuwa mishale yako imenichoma,

na mkono wako umenishukia.

38:3 Mit 3:8; 4:22; Ay 33:19Hakuna afya mwilini mwangu

kwa sababu ya ghadhabu yako,

mifupa yangu haina uzima

kwa sababu ya dhambi zangu.

38:4 Za 40:12; 65:3; Hes 11:14; Ezr 9:6; Lk 11:46Maovu yangu yamenifunika

kama mzigo usiochukulika.

38:5 Za 147:3; Ay 19:17; Za 69:5; Mit 5:23; 12:23; 13:16; Mhu 10:3Majeraha yangu yameoza na yananuka,

kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu.

38:6 Za 57:6; 145:14; 146:8; 35:14Nimeinamishwa chini na kushushwa sana,

mchana kutwa nazunguka nikiomboleza.

38:7 Ay 14:22; 7:5Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo,

hakuna afya mwilini mwangu.

38:8 Za 6:3, 6; 22:1; 34:18; Mit 17:22; 5:11Nimedhoofika na kupondwa kabisa,

nasononeka kwa maumivu makuu ya moyoni.

38:9 Za 119:20; 143:7; Ay 3:24Ee Bwana, yote ninayoyaonea shauku

yako wazi mbele zako,

kutamani kwangu sana

hakufichiki mbele zako.

38:10 Ay 37:1; Za 6:7; 31:10; 19:8; 88:9Moyo wangu unapigapiga,

nguvu zangu zimeniishia;

hata macho yangu yametiwa giza.

38:11 Za 38:5; Lk 10:31Rafiki na wenzangu wananikwepa

kwa sababu ya majeraha yangu;

majirani zangu wanakaa mbali nami.

Read More of Zaburi 38