Zaburi 37:32-40 NEN

Zaburi 37:32-40

37:32 Za 10:8; 11:5Watu waovu huvizia wenye haki,

wakitafuta kuwaua;

37:33 Ay 32:3; 2Pet 2:9; Za 109:31; 34:22; 79:11; 2:9lakini Bwana hatawaacha mikononi mwao

wala hatawaacha wahukumiwe

kuwa wakosa wanaposhtakiwa.

37:34 Za 27:14; 18:21; 52:6Mngojee Bwana,

na uishike njia yake.

Naye atakutukuza uirithi nchi,

waovu watakapokatiliwa mbali,

utaliona hilo.

37:35 Ay 5:3Nimemwona mtu mwovu na mkatili akistawi

kama mwerezi wa Lebanoni,

37:36 Za 37:10; Dan 11:19; Mit 12:7; Isa 41:12lakini alitoweka mara na hakuonekana,

ingawa nilimtafuta, hakupatikana.

37:37 Mwa 6:9; Za 11:7; 18:25; Isa 57:1-2Watafakari watu wasio na hatia,

wachunguze watu wakamilifu,

kuna mafanikio kwa mtu apendaye amani.

37:38 Za 1:1, 2; 73:9, 19; Ay 1:1; 1The 4:17; Lk 2:25-30; Mdo 7:59, 60; 2Pet 1:14; Isa 32:17; 2Tim 4:6-8Lakini watenda dhambi wote wataangamizwa,

mafanikio yao yatakatiliwa mbali.

37:39 Isa 12:2; Yon 2:8; Za 3:8; 9:9Wokovu wa wenye haki hutoka kwa Bwana,

yeye ni ngome yao wakati wa shida.

37:40 1Nya 5:20; Dan 3:17; Za 20:2; 18:48; 2:12; 34:7Bwana huwasaidia na kuwaokoa,

huwaokoa kutoka kwa waovu na kuwahifadhi,

kwa maana wanamkimbilia.

Read More of Zaburi 37