Zaburi 35:19-28 NEN

Zaburi 35:19-28

35:19 Za 9:13; 38:19; 69:4; Yn 15:25; Mit 6:13; 10:10Usiwaache wale wanaonisimanga,

wale ambao ni adui zangu bila sababu;

usiwaache wale ambao ni adui zangu bila sababu

wakonyeze jicho kwa hila.

35:20 Za 38:12; 55:21; Yer 9:8; Mik 6:12Hawazungumzi kwa amani,

bali wanatunga mashtaka ya uongo

dhidi ya wale wanaoishi

kwa utulivu katika nchi.

35:21 Ay 16:10; Eze 25:3; Za 40:15; 70:3Hunifumbulia vinywa vyao wakisema, “Aha! Aha!

Kwa macho yetu wenyewe tumeliona.”

35:22 Kut 3:7; Za 10:1, 14Ee Bwana, umeona hili, usiwe kimya.

Usiwe mbali nami, Ee Bwana.

35:23 Za 7:6; 80:2; 17:13; 1Sam 24:15Amka, inuka unitetee!

Unipiganie Mungu wangu na Bwana wangu.

35:24 Za 22:17; 7:8; 26:11; 2The 1:6Nihukumu kwa haki yako, Ee Bwana Mungu wangu,

sawasawa na haki yako;

usiwaache wakusimange.

35:25 Mit 1:12; Za 35:21; 124:3; Mao 2:16Usiwaache wafikiri, “Aha, hili ndilo tulilotaka!”

Au waseme, “Tumemmeza.”

35:26 Za 22:17; 4:1; 109:29; 38:16; Ay 8:22; 19:5; Mik 7:10Wote wanaofurahia dhiki yangu

waaibishwe na wachanganyikiwe;

hao wanaojiinua dhidi yangu

wavikwe aibu na dharau.

35:27 Za 9:4; 20:5; 33:3; 147:11; 149:4; Ay 17:3Wale wanaofurahia hukumu yangu ya haki

wapige kelele za shangwe na furaha;

hebu waseme siku zote, “Bwana atukuzwe,

ambaye amefurahia mafanikio ya mtumishi wake.”

35:28 Za 5:8; 51:14; 71:15, 24; 72:15Ulimi wangu utanena haki yako

na sifa zako mchana kutwa.

Read More of Zaburi 35