Zaburi 35:1-10 NEN

Zaburi 35:1-10

Zaburi 35

Kuomba Msaada: Kuokolewa Kutokana Na Maadui

Zaburi ya Daudi.

35:1 1Sam 24:15; Kut 14:14Ee Bwana, pingana na wale wanaopingana nami,

upigane na hao wanaopigana nami.

35:2 Za 3:3, 7; Ay 17:3; Mwa 50:24; 35:3; Hes 25:7; Za 27:1; Yos 8:18Chukua ngao na kigao.

Inuka unisaidie.

Inua mkuki wako na fumo35:3 Fumo ni sawa na sagai, maana yake ni mkuki mfupi. lako

dhidi ya hao wanaonifuatia.

Iambie nafsi yangu,

“Mimi ni wokovu wako.”

35:4 Za 38:12; 40:14; 69:6, 19; 70:2; 83:17; 25:3; 129:5; Yer 4:30; Mal 2:9; Isa 45:16Wafedheheshwe na waaibishwe

wale wanaotafuta uhai wangu.

Wanaofanya shauri kuniangamiza

warudishwe nyuma kwa hofu.

35:5 Ay 13:25; Za 1:4; 34:7Wawe kama makapi yapeperushwayo na upepo,

malaika wa Bwana akiwafukuza.

Njia yao na iwe giza na ya utelezi,

malaika wa Bwana akiwafuatilia.

35:7 Ay 18:8; 9:31; Za 7:4; 7:15; 55:23Kwa vile walinifichia wavu wao bila sababu,

na bila sababu wamenichimbia shimo,

35:8 Isa 47:11; 1The 5:3; Za 7:15; Mit 5:22maafa na yawapate ghafula:

wavu walionifichia na uwatege wenyewe,

na waanguke katika shimo hilo,

kwa maangamizo yao.

35:9 Za 2:11; 9:14; 13:5; 27:1; Lk 1:47; 1Sam 2:1; Isa 61:10; Ebr 3:18Ndipo nafsi yangu itashangilia katika Bwana

na kuufurahia wokovu wake.

35:10 Kut 9:14; Za 12:5; 71:19; 18:17, 31; 113:5; 37:14; 86:1; 74:21; 109:16; 140:12; Isa 41:17Nitapaza sauti yangu nikisema,

“Ni nani aliye kama wewe, Ee Bwana?

Wewe huwaokoa maskini kutokana na wale walio na nguvu kuliko wao,

maskini na mhitaji kutokana na wanaowanyangʼanya!”

Read More of Zaburi 35