Zaburi 34:1-10
Zaburi 3434 Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
Sifa Na Wema Wa Mungu
Zaburi ya Daudi, alipojifanya mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimfukuza, naye akaondoka.
34:1 Za 71:6; Efe 5:20; 1The 5:18Nitamtukuza Bwana nyakati zote,
sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote.
34:2 Za 44:8; 69:32; 107:42; 119:74; Yer 9:24; 1Kor 1:31Nafsi yangu itajisifu katika Bwana,
walioonewa watasikia na wafurahi.
34:3 Za 63:3; 86:12; Dan 4:37; Kut 15:2; Yn 17:1; Rum 15:6Mtukuzeni Bwana pamoja nami,
naam, na tulitukuze jina lake pamoja.
34:4 Za 18:6; 77:2; 18:43; 22:4; 56:13; 86:13; Kut 32:11; Yon 2:2; Mt 7:7; Lk 11:9Nilimtafuta Bwana naye akanijibu,
akaniokoa kwenye hofu zangu zote.
34:5 Kut 34:29; Za 25:3; 44:15; 69:7; 83:16Wale wamtazamao hutiwa nuru,
nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.
34:6 Za 25:17; 2Sam 22:1Maskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia,
akamwokoa katika taabu zake zote.
34:7 Mwa 32:1; Ebr 1:14; Dan 3:28; 6:22; Mt 18:10; Isa 31:5; Za 22:4; 37:40; 41:1; 97:10; Mdo 12:11; 2Fal 16:17Malaika wa Bwana hufanya kituo
akiwazunguka wale wamchao,
naye huwaokoa.
34:8 Ebr 6:5; 1Pet 2:3; Za 2:12Onjeni mwone kwamba Bwana ni mwema,
heri mtu yule anayemkimbilia.
34:9 Flp 4:19; Za 23:1; Kum 6:13; Ufu 14:7Mcheni Bwana enyi watakatifu wake,
kwa maana wale wamchao
hawapungukiwi na chochote.
34:10 Za 23:1Wana simba wenye nguvu
hutindikiwa na kuona njaa,
bali wale wamtafutao Bwana
hawatakosa kitu chochote kilicho chema.