Zaburi 33:1-11
Zaburi 33
Ukuu Na Wema Wa Mungu
33:1 Za 64:10; 101:1; 147:1; 11:7Mwimbieni Bwana kwa furaha, enyi wenye haki;
kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.
33:2 Mwa 4:21; 1Kor 14:7; Ufu 5:8; Za 92:3; 144:9Msifuni Bwana kwa kinubi,
mwimbieni sifa kwa zeze la nyuzi kumi.
33:3 Za 40:3; 35:27; 47:1; Isa 42:10; Ufu 5:9; Ay 3:7Mwimbieni wimbo mpya;
pigeni kwa ustadi, na mpaze sauti za shangwe.
33:4 Ufu 19:9; 22:6; Za 19:8; 18:25; 119:142; 25:10Maana neno la Bwana ni haki na kweli,
ni mwaminifu kwa yote atendayo.
33:5 Za 11:7; 6:4Bwana hupenda uadilifu na haki;
dunia imejaa upendo wake usiokoma.
33:6 Ebr 11:3; Kut 8:19; Mwa 1:3, 16; 2Nya 2:12; Yn 1:1-3; Ay 26:13Kwa neno la Bwana mbingu ziliumbwa,
jeshi lao la angani kwa pumzi ya kinywa chake.
33:7 Mwa 1:10; Yos 3:16Ameyakusanya maji ya bahari
kama kwenye chungu;
vilindi vya bahari
ameviweka katika ghala.
33:8 Kum 6:13; 14:23; Za 2:11; 49:1; Isa 18:3; Mik 1:2Dunia yote na imwogope Bwana,
watu wote wa dunia wamche.
33:9 Za 148:5; Mwa 1:3Kwa maana Mungu alisema, na ikawa,
aliamuru na ikasimama imara.
33:10 Isa 44:25; Za 2:1; Ay 5:12Bwana huzuia mipango ya mataifa,
hupinga makusudi ya mataifa.
33:11 Hes 23:19; Yer 51:12, 29; Ay 23:13; Mit 19:21; Eze 38:10; Mdo 4:27, 28Lakini mipango ya Bwana inasimama imara milele,
makusudi ya moyo wake kwa vizazi vyote.