Zaburi 31:9-18 NEN

Zaburi 31:9-18

31:9 Za 4:1; 6:7; 63:1Ee Bwana unihurumie, kwa kuwa niko kwenye shida;

macho yangu yanafifia kwa huzuni,

nafsi yangu na mwili wangu kwa sikitiko.

31:10 Za 6:6; 22:5; 32:4; 38:10; 73:26; 25:18; 6:2Maisha yangu yamedhoofika kwa majonzi,

naam, miaka yangu kwa kulia kwa maumivu makali;

nguvu zangu zinaisha kwa ajili ya mateso,

na mifupa yangu inachakaa.

31:11 Kum 30:7; Za 3:7; 25:19; 102; 22:6; 38:11; 88:8Kwa sababu ya adui zangu wote,

nimedharauliwa kabisa na jirani zangu,

hata kwa rafiki zangu nimekuwa tisho,

wale wanionao barabarani hunikimbia.

31:12 Za 28:1; 88:4Nimesahaulika miongoni mwao kama mtu aliyekufa,

nimekuwa kama chombo cha mfinyanzi kilichovunjika.

31:13 Law 19:16; Isa 13:8; Za 50:20; 41:7; 56:6; 71:10; 83:3; Ay 18:11; Yer 6:25; 20:3, 10; 46:5; 49:5; Mao 2:22; Mwa 37:18; Mt 12:14; 27:1Kwa maana nimesikia maneno niliyosingiziwa na wengi;

vitisho viko pande zote;

kwa kuwa wamefanya mashauri dhidi yangu,

na kula njama kuniua.

31:14 Za 4:5Lakini mimi ninakutumaini wewe peke yako, Ee Bwana;

nimesema, “Wewe ndiwe Mungu wangu.”

31:15 Ay 14:5Siku za maisha yangu ziko mikononi mwako,

uniokoe mikononi mwa adui zangu

na wale wanifuatiao.

31:16 Hes 6:25; Dan 9:17; Za 4:6; 6:4Mwangazie mtumishi wako uso wako,

uniokoe kwa ajili ya upendo wako usiokoma.

31:17 Za 22:5; 94:17; 115:17; 25:2; 1Sam 2:9Usiniache niaibike, Ee Bwana,

kwa maana nimekulilia wewe,

bali waovu waaibishwe

na kunyamazishwa Kuzimu.

31:18 Za 120:2; 12:3; Mit 10:18; 26:24; 1Sam 2:3; Yud 15Midomo yao isemayo uongo na inyamazishwe,

kwa maana kwa kiburi na dharau

wao husema kwa majivuno

dhidi ya wenye haki.

Read More of Zaburi 31