Zaburi 31:19-24 NEN

Zaburi 31:19-24

31:19 Za 27:13; 23:5; Isa 64:4; 1Kor 2:9; Rum 11:22Tazama jinsi ulivyo mkuu wema wako,

uliowawekea akiba wakuchao,

ambao huwapa wale wakukimbiliao

machoni pa watu.

31:20 Za 55:8; 27:5; 17:8; Mwa 37:18; Ay 5:21Unawahifadhi katika uvuli wa uwepo wako

kutokana na hila za wanadamu;

katika makao yako huwaweka salama

kutokana na ndimi za mashtaka.

31:21 Za 28:6; 17:7; 1Sam 23:7Atukuzwe Bwana,

kwa kuwa amenionyesha upendo wake wa ajabu

nilipokuwa katika mji uliozingirwa.

31:22 Za 116:11; 37:9; 88:5; 6:9; 66:19; 116:1; 145:19; Ay 6:9; 17:1; Isa 38:12Katika hofu yangu nilisema,

“Nimekatiliwa mbali na macho yako!”

Hata hivyo ulisikia kilio changu

ukanihurumia nilipokuita unisaidie.

31:23 Za 4:3; 94:2; 18:25; Ufu 2:10; Kum 32:41; 1Pet 1:5Mpendeni Bwana ninyi watakatifu wake wote!

Bwana huwahifadhi waaminifu,

lakini wenye kiburi huwalipiza kikamilifu.

31:24 Za 27:14Kuweni hodari na mjipe moyo,

ninyi nyote mnaomtumaini Bwana.

Read More of Zaburi 31