Zaburi 29:1-11
Zaburi 29
Sauti Ya Bwana Wakati Wa Dhoruba
Zaburi ya Daudi.
29:1 1Nya 16:28; 2Sam 1:19; Isa 10:13; Za 103:20; 8:1Mpeni Bwana, enyi mashujaa,
mpeni Bwana utukufu na nguvu.
29:2 1Nya 16:29; Za 96:7-9Mpeni Bwana utukufu unaostahili jina lake;
mwabuduni Bwana katika uzuri wa utakatifu wake.
29:3 Ay 37:5; Za 24:7; 18:13; 46:6; 68:33; 77:17; Mdo 7:2; 1Sam 2:10; Yer 10:13; 25:30; Yoe 2:11; Amo 1:2; Kut 15:10Sauti ya Bwana iko juu ya maji;
Mungu wa utukufu hupiga radi,
Bwana hupiga radi juu ya maji makuu.
29:4 Za 68:33Sauti ya Bwana ina nguvu;
sauti ya Bwana ni tukufu.
29:5 Amu 9:15Sauti ya Bwana huvunja mierezi;
Bwana huvunja vipande vipande
mierezi ya Lebanoni.
29:6 Za 92:10; 114:4; Kum 3:9; Ay 39:9; Hes 23:22Hufanya Lebanoni irukaruke kama ndama,
Sirioni29:6 Yaani Mlima Hermoni. urukaruke kama mwana nyati.
29:7 Eze 1:14; Ufu 8:5Sauti ya Bwana hupiga kwa miali
ya umeme wa radi.
29:8 Hes 13:26; 20:1Sauti ya Bwana hutikisa jangwa;
Bwana hutikisa Jangwa la Kadeshi.
29:9 Isa 2:13; Eze 27:6; Amo 2:9; Za 26:8Sauti ya Bwana huzalisha ayala,
na huuacha msitu wazi.
Hekaluni mwake wote wasema,
“Utukufu!”
29:10 Mwa 6:17; Kut 15:18Bwana huketi akiwa ametawazwa juu ya gharika;
Bwana ametawazwa kuwa Mfalme milele.
29:11 Za 18:1; 28:8; 68:35; Law 26:6; Hes 6:26; Isa 40:29Bwana huwapa watu wake nguvu;
Bwana huwabariki watu wake kwa kuwapa amani.