Zaburi 27:7-14
27:7 Za 4:1; 5:3; 18:6; 55:17; 119:149; 130:2; Isa 28:23Isikie sauti yangu nikuitapo, Ee Bwana,
unihurumie na unijibu.
27:8 1Nya 16:11Moyo wangu unasema kuhusu wewe,
“Utafute uso wake!”
Uso wako, Bwana “Nitautafuta.”
27:9 Za 2:5; 119:8; 18:46; 22:24; 37:28; Mwa 49:25; Kum 31:17; 33:29; 4:31; Isa 41:17; 62:12; Yer 14:9Usinifiche uso wako,
usimkatae mtumishi wako kwa hasira;
wewe umekuwa msaada wangu.
Usinikatae wala usiniache,
Ee Mungu Mwokozi wangu.
Hata kama baba yangu na mama wakiniacha,
Bwana atanipokea.
27:11 Ezr 8:21; Za 5:8; 72:4; 78:42; 106:10; Yer 21:12; Kut 33:13Nifundishe njia yako, Ee Bwana,
niongoze katika njia iliyonyooka
kwa sababu ya watesi wangu.
27:12 Kum 19:16; Mt 26:60; Mdo 6:13; 1Kor 15:15Usiniachilie kwa nia za adui zangu,
kwa maana mashahidi wa uongo
wameinuka dhidi yangu,
wakipumua ujeuri.
27:13 Kut 33:19; 2Nya 6:41; Za 33:6; 31:19; 145:7; Ay 18:13Nami bado nina tumaini hili:
nitauona wema wa Bwana
katika nchi ya walio hai.
27:14 Efe 6:10; Amu 5:21; Kum 1:21; Sef 3:8; Hab 2:3; Za 33:20; 130:5, 6; Mdo 1:4; Isa 8:17; 30:18Mngojee Bwana,
uwe hodari na mwenye moyo mkuu,
nawe, umngojee Bwana.