Zaburi 27:1-6 NEN

Zaburi 27:1-6

Zaburi 27

Sala Ya Kusifu

Zaburi ya Daudi.

27:1 2Sam 22:29; Ay 13:5; Za 3:8; 9:9; 56:4, 11; 118:6; Kut 15:2Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu,

nimwogope nani?

Bwana ni ngome ya uzima wangu,

nimhofu nani?

27:2 Za 9:3; 20:8; 37:24; Dan 11:19; Rum 11:11Waovu watakaposogea dhidi yangu

ili wanile nyama yangu,

adui zangu na watesi wangu watakaponishambulia,

watajikwaa na kuanguka.

27:3 Mwa 4:7; Za 3:6; Ay 4:6Hata jeshi linizunguke pande zote,

moyo wangu hautaogopa;

hata vita vitokee dhidi yangu,

hata hapo nitakuwa na ujasiri.

27:4 Lk 10:42; Za 23:6; 61:4Jambo moja ninamwomba Bwana,

hili ndilo ninalolitafuta:

niweze kukaa nyumbani mwa Bwana

siku zote za maisha yangu,

niutazame uzuri wa Bwana

na kumtafuta hekaluni mwake.

27:5 Ay 38:23; Za 12:7, 8; 40:2Kwa kuwa siku ya shida,

atanihifadhi salama katika maskani yake,

atanificha uvulini mwa hema yake

na kuniweka juu kwenye mwamba.

27:6 2Sam 22:49; Za 3:3; 33:2; 54:6; 18:48; 22:12; 92:1; 50:14; 107:22; 116:17; 147:7; Ezr 3:13; Ay 22:26; Kut 15:1; Efe 5:19Kisha kichwa changu kitainuliwa

juu ya adui zangu wanaonizunguka.

Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe;

nitamwimbia Bwana na kumsifu.

Read More of Zaburi 27