Zaburi 25:8-15 NEN

Zaburi 25:8-15

25:8 Za 32:8; 92:15; Isa 26:7; 28:26Bwana ni mwema na mwenye adili,

kwa hiyo huwafundisha wenye dhambi njia zake.

25:9 Za 23:3, 4; 18:25; 103:18; 132:12Huwaongoza wanyenyekevu katika haki,

naye huwafundisha njia yake.

25:10 Za 18:25; 103:18; 132:12Njia zote za Bwana ni za upendo na uaminifu

kwa wale wanaoshika shuhuda za agano lake.

25:11 Kut 9:16; Za 31:3; 79:9; 34:9; Kut 32:30; Za 78:38; Yer 14:7Ee Bwana, kwa ajili ya jina lako,

unisamehe uovu wangu, ijapokuwa ni mwingi.

25:12 Ay 1:8Ni nani basi, mtu yule anayemcha Bwana?

Atamfundisha katika njia

atakayoichagua kwa ajili yake.

25:13 Kum 30:15; Mt 5:5; Ay 8:7; 1Fal 3:14; Hes 14:24Mtu huyo atafanikiwa maishani mwake,

nao wazao wake watairithi nchi.

25:14 Mit 3:32; Yn 7:17; Mwa 17:2Siri ya Bwana iko kwa wale wamchao,

yeye huwajulisha agano lake.

25:15 2Nya 20:12; Za 119:110; 123:2; Ebr 12:2; Ay 34:30Macho yangu humwelekea Bwana daima,

kwa kuwa yeye peke yake ndiye ataitoa

miguu yangu kutoka mtego.

Read More of Zaburi 25