Zaburi 25:1-7 NEN

Zaburi 25:1-7

Zaburi 2525 Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.

Kumwomba Mungu Uongozi Na Ulinzi

Zaburi ya Daudi.

25:1 Za 86:4; 143:8Kwako wewe, Ee Bwana,

nainua nafsi yangu,

25:2 Za 31:6; 143:8ni wewe ninayekutumainia,

Ee Mungu wangu.

Usiniache niaibike,

wala usiache adui zangu wakanishinda.

25:3 Za 22:5; 2Tim 3:4; Isa 29:22; 24:16; Hab 1:13; Sef 3:4Kamwe hakuna hata mmoja anayekutegemea

atakayeaibishwa,

bali wataaibishwa

wafanyao hila bila sababu.

25:4 Ay 34:32Nionyeshe njia zako, Ee Bwana,

nifundishe mapito yako,

25:5 Za 31:3; 43:3; Yn 16:13niongoze katika kweli yako na kunifundisha,

kwa maana wewe ni Mungu Mwokozi wangu,

nalo tumaini langu liko kwako wakati wote.

25:6 Za 5:7; 98:3; Isa 63:7, 15; Yer 31:20; Hos 11:8Kumbuka, Ee Bwana, rehema zako kuu na upendo,

kwa maana zimekuwepo tangu zamani.

25:7 Ay 13:26; Isa 54:4; Yer 3:25; 31:19; 32:30; 2Tim 2:22; Eze 16:22, 60; 23:3; Za 34:8; 83:1; 107:17; 6:4; 51:1; 69:16; 109:26; 119:124; Kut 3:21; 1Nya 16:34Usizikumbuke dhambi za ujana wangu

wala njia zangu za uasi,

sawasawa na upendo wako unikumbuke,

kwa maana wewe ni mwema, Ee Bwana.

Read More of Zaburi 25