Zaburi 21:8-13 NEN

Zaburi 21:8-13

21:8 Isa 10:10Mkono wako utawashika adui zako wote,

mkono wako wa kuume utawakamata adui zako.

21:9 Kum 32:22; Yer 15:14Wakati utakapojitokeza

utawafanya kama tanuru ya moto.

Katika ghadhabu yake Bwana atawameza,

moto wake utawateketeza.

21:10 Kum 28:18Utawaangamiza wazao wao kutoka duniani,

uzao wao kutoka wanadamu.

21:11 Za 2:1; 10:2; 26:10; 37:7; Ay 10:3Ingawa watapanga mabaya dhidi yako

na kutunga hila, hawawezi kufanikiwa,

21:12 Kut 23:27kwa kuwa utawafanya wakimbie

utakapowalenga usoni pao

kwa mshale kutoka kwenye upinde wako.

21:13 Za 18:46; Ufu 15:3, 4Ee Bwana, utukuzwe katika nguvu zako,

tutaimba na kusifu nguvu zako.

Read More of Zaburi 21