Zaburi 21:1-7 NEN

Zaburi 21:1-7

Zaburi 21

Shukrani Kwa Mungu Kwa Ajili Ya Ushindi

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

21:1 1Sam 2:10; 2Sam 22:51Ee Bwana, mfalme huzifurahia nguvu zako.

Tazama jinsi ilivyo kuu furaha yake

kwa ushindi unaompa!

21:2 Za 20:4; Yn 11:42Umempa haja ya moyo wake

na hukumzuilia maombi ya midomo yake.

21:3 2Sam 12:30; Ufu 14:14; Zek 6:11Ulimkaribisha kwa baraka tele

na kumvika taji ya dhahabu safi kichwani pake.

21:4 Za 10:16; 45:17; 48:14; 133:3; 2Sam 7:19Alikuomba maisha, nawe ukampa,

wingi wa siku milele na milele.

21:5 Za 18:50; 44:4; 8:5; 45:3; 93:1; 96:6; 104:1Kutokana na ushindi uliompa, utukufu wake ni mkubwa,

umeweka juu yake fahari na utukufu.

21:6 Za 43:4; 126:3; 1Nya 17:27Hakika umempa baraka za milele,

umemfanya awe na furaha

kwa shangwe ya uwepo wako.

21:7 2Fal 18:5; Za 6:4; 15:5; 55:22; 91:7; Mwa 14:18Kwa kuwa mfalme anamtumaini Bwana;

kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.

Read More of Zaburi 21