Zaburi 19:7-14 NEN

Zaburi 19:7-14

19:7 Yak 1:25; Kum 4:6; Za 1:2; 23:3; 93:5; 119:130, 138, 142, 144; 11:7Sheria ya Bwana ni kamilifu,

ikihuisha nafsi.

Shuhuda za Bwana ni za kuaminika,

zikimpa mjinga hekima.

19:8 Za 33:4; 38:10; 119:14, 128; Ezr 9:7; Neh 9:13; Rum 7:12Maagizo ya Bwana ni kamili,

nayo hufurahisha moyo.

Amri za Bwana huangaza,

zatia nuru machoni.

19:9 Mhu 12:13; Isa 33:6; Za 34:11; 111:10; 119:138; Mit 1:7Kumcha Bwana ni utakatifu,

nako kwadumu milele.

Amri za Bwana ni za hakika,

nazo zina haki.

19:10 Ay 22:24; Eze 3:3; Mit 8:10; 1Sam 14:27; Za 119:72, 103Ni za thamani kuliko dhahabu,

kuliko dhahabu iliyo safi sana,

ni tamu kuliko asali,

kuliko asali kutoka kwenye sega.

19:11 Mit 6:22Kwa hizo mtumishi wako anaonywa,

katika kuzishika kuna thawabu kubwa.

19:12 Za 51:2; 90:8; Mhu 12:14Ni nani awezaye kutambua makosa yake?

Nisamehe makosa yangu nisiyoyajua.

19:13 Hes 15:30; Mwa 6:9; Za 18:32; 119:133Mlinde mtumishi wako na dhambi za makusudi,

nazo zisinitawale.

Ndipo nitakapokuwa sina lawama,

wala sitakuwa na hatia ya kosa kubwa.

19:14 Za 104:34; 18:31; Kut 6:6; Isa 44:6; Ay 19:25Maneno ya kinywa changu

na mawazo ya moyo wangu,

yapate kibali mbele zako, Ee Bwana,

Mwamba wangu na Mkombozi wangu.

Read More of Zaburi 19