Zaburi 19:1-6 NEN

Zaburi 19:1-6

Zaburi 19

Utukufu Wa Mungu Katika Uumbaji

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

19:1 Isa 6:3; 40:22; Za 4:2; 97:6; 89:5; 50:6; 8:1, 6; 148:3; 103:22; Rum 1:19; Mwa 1:8Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu,

anga zahubiri kazi ya mikono yake.

19:2 Za 74:16Siku baada ya siku zinatoa habari,

usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa.

Hakuna msemo wala lugha,

ambapo sauti zao hazisikiki.

19:4 Rum 10:18; Za 104:2; Ay 36:29; Amu 5:31Sauti yao imeenea duniani pote,

nayo maneno yao yameenea

hadi miisho ya ulimwengu.

Katika mbingu amepiga hema kwa ajili ya jua,

19:5 1Sam 17:4; Mhu 11:7; Yoe 2:16; Ay 36:29linafanana na bwana arusi

akitoka chumbani mwake,

kama shujaa afurahiavyo

kukamilisha kushindana kwake.

19:6 Kum 30:4; Za 11:3; Mhu 1:5Huchomoza upande mmoja wa mbingu,

na kufanya mzunguko wake

hadi upande mwingine.

Hakuna kilichojificha joto lake.

Read More of Zaburi 19