Zaburi 18:7-15 NEN

Zaburi 18:7-15

18:7 Za 97:4; Isa 5:25; 64:3; Amu 5:4, 5; Ay 9:5; Yer 10:10; Mdo 4:31Dunia ilitetemeka na kutikisika,

misingi ya milima ikatikisika,

vilitetemeka kwa sababu alikuwa amekasirika.

18:8 Ay 41:20, 21; Kut 15:17; 19:18; Mit 25:22; Za 50:3; 97:3; Dan 7:10; Rum 12:20Moshi ukapanda kutoka puani mwake,

moto uteketezao ukatoka kinywani mwake,

makaa ya moto yawakayo

yakatoka ndani mwake.

18:9 Mwa 11:5; Isa 64:1; Za 57:3; 104:3; Kut 20:21; Kum 33:26Akazipasua mbingu akashuka chini,

mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.

18:10 Mwa 3:24; Eze 10:18; Kum 33:26; Za 104:3; 99:1Alipanda juu ya kerubi akaruka,

akapaa juu kwa mbawa za upepo.

18:11 Za 97:2; Kut 19:9; Ay 22:14; Isa 4:5; Kum 4:11; Yer 43:10Alifanya giza kuwa kitu chake cha kujifunika,

hema lake kumzunguka,

mawingu meusi ya mvua ya angani.

18:12 Za 104:2; Yos 10:10; Ay 36:30Kutokana na mwanga wa uwepo wake

mawingu yalisogea,

ikanyesha mvua ya mawe

na umeme wa radi.

18:13 Kut 9:23; Za 29:3; 2Sam 2:10Bwana alinguruma kutoka mbinguni,

sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.

18:14 Kum 32:23; Ay 6:4; 36:30; Ufu 4:5; Za 21:12; Amu 4:15; Hes 24:8Aliipiga mishale yake na kutawanya adui,

naam, umeme mwingi wa radi na kuwafukuza.

18:15 Za 11:3; 76:6; 104:7; 106:9; Isa 50:2; Kut 15:8Mabonde ya bahari yalifunuliwa,

na misingi ya dunia ikawa wazi

kwa kukaripia kwako, Ee Bwana,

kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwako.

Read More of Zaburi 18