Zaburi 18:43-50 NEN

Zaburi 18:43-50

18:43 2Sam 8:1-14; Isa 55:5Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu;

umenifanya kuwa kiongozi wa mataifa,

watu ambao sikuwajua wananitumikia.

18:44 Za 144:7, 11; 54:3; Isa 25:5Mara wanisikiapo hunitii,

wageni hunyenyekea mbele yangu.

18:45 2Kor 4:1; Ebr 12:3; 1Sam 17:32; Isa 66:2; Hos 3:5; 11:10; Za 9:9; Mik 7:17Wote wanalegea,

wanatoka katika ngome zao wakitetemeka.

18:46 Yos 3:10; 2Kor 13:4; 1Sam 14:39; Kut 33:22; Za 21:13; 35:27; 40:16; 108:5; 1Nya 16:35; Lk 1:47; Yer 10:10Bwana yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu!

Atukuzwe Mungu Mwokozi wangu!

18:47 Mwa 4:24; Za 18:29; Amu 4:23Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi,

awatiishaye mataifa chini yangu,

18:48 Dan 3:17; Za 7:10; 37:40; 140:2; 18:49aniokoaye na adui zangu.

Uliniinua juu ya adui zangu;

uliniokoa toka kwa watu wajeuri.

18:49 Za 101:1; 7:17; 9:2; 108:1; 146:2; Rum 15:9Kwa hiyo nitakusifu katikati ya mataifa, Ee Bwana;

nitaliimbia sifa jina lako.

18:50 2Sam 23:1; Za 144:10; 89:4Humpa mfalme wake ushindi mkuu,

huonyesha fadhili zake kwa mpakwa mafuta wake,

kwa Daudi na wazao wake milele.

Read More of Zaburi 18