Zaburi 18:37-42 NEN

Zaburi 18:37-42

18:37 Law 26:7Niliwafuatia adui zangu na nikawapata,

sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa.

18:38 Za 68:21; 110:6; 36:12; 47:3; 140:10; Isa 26:14Niliwaseta hata hawakuweza kuinuka tena;

walianguka chini ya miguu yangu.

18:39 Za 18:32, 47; Isa 45:5, 24; Za 47:3; 144:2Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita;

uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu.

18:40 Yos 7:12; Za 18:37Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia,

nami nikawaangamiza adui zangu.

18:41 2Fal 14:26; Za 50:22; 1Sam 8:18; 14:37; Yer 11:11; Mit 1:28Walipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa;

walimlilia Bwana, lakini hakuwajibu.

18:42 Kum 9:21; Isa 2:22Niliwaponda kama mavumbi yanayopeperushwa na upepo;

niliwamwaga nje kama tope barabarani.

Read More of Zaburi 18