Zaburi 147:12-20 NEN

Zaburi 147:12-20

147:12 Za 48:1Mtukuze Bwana, ee Yerusalemu,

msifu Mungu wako, ee Sayuni,

147:13 Kum 33:25; Law 25:21; Za 128:5; 134:3kwa maana huimarisha makomeo ya malango yako

na huwabariki watu wako walio ndani yako.

147:14 Law 26:6; 2Sam 7:10; Isa 48:18; Za 132:15; Kum 32:14Huwapa amani mipakani mwenu

na kukushibisha kwa ngano safi kabisa.

147:15 Ay 37:12; Za 33:9; 148:5; Isa 55:11Hutuma amri yake duniani,

neno lake hukimbia kasi.

147:16 Za 148:8; Ay 37:12; 38:29Anatandaza theluji kama sufu

na kutawanya umande kama majivu.

147:17 Kut 9:22, 23; Ay 38:22; Za 78:47Huvurumisha mvua yake ya mawe kama changarawe.

Ni nani awezaye kustahimili ukali wa baridi yake?

147:18 Za 33:9; 107:20; 50:3Hutuma neno lake na kuviyeyusha,

huvumisha upepo wake, nayo maji hutiririka.

147:19 Kut 20:1; Mal 4:4; Za 78:5; Yos 1:8; Kum 33:4; 2Fal 22:8; Rum 3:2; 9:4Amemfunulia Yakobo neno lake,

sheria zake na maagizo yake kwa Israeli.

147:20 Rum 3:1-2; Kum 4:7-8, 32-34; Za 79:6; 103:1; 33:2; Mdo 14:16Hajafanya hivyo kwa taifa lingine lolote,

hawazijui sheria zake.

Msifuni Bwana.

Read More of Zaburi 147