Zaburi 145:13-21 NEN

Zaburi 145:13-21

145:13 Kut 15:18; 1Tim 1:17; 2Pet 1:11; Ufu 11:15; Kum 7:9; 1Kor 1:9; Yos 23:14Ufalme wako ni ufalme wa milele,

mamlaka yako hudumu vizazi vyote.

Bwana ni mwaminifu kwa ahadi zake zote

na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.

145:14 Za 37:17; 146:8; 38:6; 1Sam 2:8Bwana huwategemeza wote waangukao,

na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao.

145:15 Mwa 1:30; Ay 28:5; Mt 6:26; Za 37:25Macho yao wote yanakutazama wewe,

nawe huwapa chakula chao wakati wake.

145:16 Za 90:14; 104; 28Waufumbua mkono wako,

watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai.

145:17 Kut 9:27; Ezr 9:15Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote,

na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.

145:18 Flp 4:5; Za 46:1; 18:6; 80:18; 91:1; Isa 61:10; Ufu 3:20; Yak 4:8; 1Yn 2:24; Yud 23; Yn 4:23; 14:23; Hes 23:21Bwana yu karibu na wote wamwitao,

karibu na wote wamwitao kwa uaminifu.

145:19 1Yn 5:14; Za 20:4; 31:22; 40:1; 7:10; 34:18; 1Sam 10:19; Ay 22:28Huwatimizia wamchao matakwa yao,

husikia kilio chao na kuwaokoa.

145:20 Za 94:23; 31:23; 91:14; 97:10; 1:6; 1Pet 1:5Bwana huwalinda wote wampendao,

bali waovu wote atawaangamiza.

145:21 Za 71:8; 65:2; 150:6; 30:4; 99:3; Kut 3:15Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana.

Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu

milele na milele.

Read More of Zaburi 145