Zaburi 140:6-13 NEN

Zaburi 140:6-13

140:6 Za 16:2; 28:2, 6Ee Bwana, ninakuambia, “Wewe ni Mungu wangu.”

Ee Bwana, usikie kilio changu na kunihurumia.

Ee Bwana Mwenyezi, Mwokozi wangu mwenye nguvu,

unikingaye kichwa changu siku ya vita:

140:8 Za 10:2-3; 66:7; Ay 5:12-13Ee Bwana, usiwape waovu matakwa yao,

usiache mipango yao ikafanikiwa,

wasije wakajisifu.

140:9 Mit 18:7Vichwa vya wanaonizunguka vifunikwe

na shida zinazosababishwa na midomo yao.

140:10 Za 11:6; 21:9; Mt 3:10; Lk 12:40; Ufu 20:15Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie!

Na watupwe motoni,

katika mashimo ya matope,

wasiinuke tena kamwe.

140:11 Za 34:21Wasingiziaji wasifanikiwe katika nchi;

maafa na yawawinde watu wenye jeuri.

140:12 1Fal 8:45; Za 35:10; 82:3; 109:31Najua kwamba Bwana huwapatia maskini haki,

na kuitegemeza njia ya mhitaji.

140:13 Za 138:2; 11:7; 16:11Hakika wenye haki watalisifu jina lako,

na waadilifu wataishi mbele zako.

Read More of Zaburi 140