Zaburi 139:17-24 NEN

Zaburi 139:17-24

139:17 Za 92:5; Ay 5:9Tazama jinsi yalivyo ya thamani mawazo yako kwangu, Ee Mungu!

Jinsi jumla yake ilivyo kubwa!

139:18 Za 40:5; 3:5; Ay 29:18Kama ningezihesabu,

zingekuwa nyingi kuliko mchanga.

Niamkapo,

bado niko pamoja nawe.

139:19 Za 5:6; 6:8; 59:2; Isa 11:4Laiti ungewachinja waovu, Ee Mungu!

Ondokeni kwangu, ninyi wamwaga damu!

139:20 Za 65:7; Kum 5:11; Ay 21:14-15; Yud 15Wanazungumza juu yako wakiwa na kusudi baya,

adui zako wanatumia vibaya jina lako.

139:21 2Nya 19:2; Za 31:6; 26:5; 119:113Ee Bwana, je, nisiwachukie wanaokuchukia?

Nisiwachukie sana wanaoinuka dhidi yako?

139:22 Mt 5:43Sina kitu zaidi ya chuki dhidi yao,

ninawahesabu ni adui zangu.

139:23 Ay 31:6; 1Sam 16:7; 1Nya 29:17; Za 7:9; Mit 17:3; Yer 11:20; Ufu 2:23Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu,

nijaribu na ujue mawazo yangu.

139:24 Yer 25:5; 36:3; Za 5:8; 23:2; 143:10Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu,

uniongoze katika njia ya milele.

Read More of Zaburi 139