Zaburi 139:11-16 NEN

Zaburi 139:11-16

Kama nikisema, “Hakika giza litanificha

na nuru inayonizunguka iwe usiku,”

139:12 Ay 34:22; Dan 2:22hata giza halitakuwa giza kwako,

usiku utangʼaa kama mchana,

kwa kuwa giza ni kama nuru kwako.

139:13 Za 119:73; Ay 10:11; Isa 44:2, 24; 46:3; 49:5; Yer 1:5Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;

uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.

Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa

kwa namna ya ajabu na ya kutisha;

kazi zako ni za ajabu,

ninajua hayo kikamilifu.

139:15 Mhu 11:5; Ay 10:11; Za 63:9Umbile langu halikufichika kwako,

nilipoumbwa mahali pa siri.

Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi,

139:16 Ay 33:29; Za 90:12macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika.

Siku zangu zote ulizonipangia

ziliandikwa katika kitabu chako

kabla haijakuwepo hata moja.

Read More of Zaburi 139