Zaburi 139:1-10 NEN

Zaburi 139:1-10

Zaburi 139

Mungu Asiyeweza Kukwepwa

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

139:1 Za 17:3; 44:21; Rum 8:27Ee Bwana, umenichunguza

na kunijua.

139:2 2Fal 19:27; Za 94:11; Mit 24:12; Yer 12:3Unajua ninapoketi na ninapoinuka;

unatambua mawazo yangu tokea mbali.

139:3 2Fal 19:27; Ay 31:4Unafahamu kutoka kwangu na kulala kwangu;

unaelewa njia zangu zote.

139:4 Ebr 4:13Kabla neno halijafika katika ulimi wangu,

wewe walijua kikamilifu, Ee Bwana.

139:5 1Sam 25:16; Za 32:10; 34:7; 125:2Umenizunguka nyuma na mbele;

umeweka mkono wako juu yangu.

139:6 Za 131:1; Rum 11:33Maarifa haya ni ya ajabu mno kwangu,

ni ya juu sana kwangu kuyafikia.

139:7 Yer 23:24Niende wapi nijiepushe na Roho yako?

Niende wapi niukimbie uso wako?

139:8 Kum 30:12-15; Amo 9:2-3; Ay 17:13Kama nikienda juu mbinguni, wewe uko huko;

nikifanya vilindi139:8 Vilindi ina maana ya Kuzimu, ambayo ni Sheol kwa Kiebrania. kuwa kitanda changu,

wewe uko huko.

Kama nikipanda juu ya mbawa za mapambazuko,

kama nikikaa pande za mbali za bahari,

139:10 Za 23:3; 108:6; Isa 41:10hata huko mkono wako utaniongoza,

mkono wako wa kuume utanishika kwa uthabiti.

Read More of Zaburi 139